Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuanze na Katiba kwanza - Mnyika

IMG 4548 John Mnyika.jpeg John Mnyika.

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ameshauri kuwa uanze mchakato wa mabadiliko ya Katiba kabla ya kubadilisha sheria ili kuzuia kuwa na sheria zinazokinzana na Katiba.

Mnyika ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 22, 2023 katika mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji, vitongoji na Uchaguzi Mkuu 2025 ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

“Baadhi ya taasisi zinanyimwa vibali vya kusimamia uchaguzi, lazima tutengeze utaratibu wa kutengeneza katiba inayowezesha hayo, na hapa nasema ni lazima tupate katiba mpya kwanza au tupeleke mswada wa marekebisho ya katiba na baada ya hapo tuendelee na sheria za uchaguzi.

“Kwasababu tukiacha hivyo tutakuwa na sheria zinazokinzana na katiba…kwahiyo lazima tufanye marekebisho ili uchaguzi wa serikali za mtaa pia uwe chini ya Tume ya Uchaguzi,” amesema Mnyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: