Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sumaye atupa dongo Chadema

Sumaye Sema Frederick Sumaye

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Frederick Sumaye amesema hakuna chama cha siasa cha upinzani kinachoweza kuendesha nchi zaidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Sumaye ametoa kauli hiyo akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Emanuel Nchimbi, uliofanyika mkoani Manyara.

Licha ya kutotaja jina, Sumaye amedai kuna chama kabla hakijapata dola kinaanza kuparurana hivyo kikipewa mamlaka hakitaweza kuongoza wananchi.

Aidha, Sumaye amesema mbali na kwenye vyama vya upinzani, lakini hata ndani ya CCM hakuna mtu anayeweza kuendesha nchi kama Rais Samia Suluhu Hassan.

Tundu Lissu

“Hakuna mtu atakayeweza kuendesha nchi kama kama Rais Samia, wacha nje ya Ccm hata ndani ya CCM hakuna. Husikii wenyewe wanaparurana hovyo hawapalata madaraka, wakipata madaraka si tutakoma?” amesema Sumaye.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hivi karibuni kilidaiwa kuingia katika mgogoro mzito baada ya makamu wake mwenyekiti bara, Tundu Lissu kudai kuna fedha chafu zinazotembezwa katika chaguzi za ndani za chama hicho.

Katika hatua nyingine, Sumaye ameitaka CCM kuhakikisha hakipotezi kata, kijiji, jimbo wala kura zake za urais katika chaguzi zijazo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live