Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Subira Mgalu amvaa Prof. Anna Tibaijuka

Subira Khamisi Mgalu Subira Mgalu amvaa Prof. Anna Tibaijuka

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti Maalumu, Subira Mgalu amemtaka Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kutopotosha umma kuhusu utaratibu uliofanyika bungeni kwenye kupitisha azimio la Bandari.

Subira ameyasema hayo jana wakati akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

“Kuna kiongozi namheshimu sana eti anasema kwa nini wabunge hatukuitwa jina mmoja mmoja kupiga kura, nataka nimwambie yeye amekaa humu ndani ya bunge kwa miaka 10 utaratibu wa kupiga kura ya kuitwa mmoja mmoja ni kupitisha bajeti ya Serikali tu lakini masuala mengine yote utaratibu ni kuhojiwa,”amesema.

“Lakini nataka nimkumbushe Profesa Tibaijuka alipokuwa Waziri (Ardhi) mwaka 2013 aliwasilisha mpango wa kuifanya mji wa Kigamboni kuwa mji wa kisasa wa thamani ya Sh11 trilioni japo haukufanikiwa lakini tuliupitisha humu bungeni kwa kura za kuhojiwa,” amesema Subira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: