Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Polisi watakiwa kuwaachilia waandishi waliokamatwa Mbeya

Tanzania: Polisi Waachia Baadhi Ya Wanachama Na Viongozi Wa Chadema.png Polisi watakiwa kuwaachilia waandishi waliokamatwa Mbeya

Tue, 13 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jukwaa la wahariri habari nchini Tanzania limetoa wito kwa vyombo vya dola kuwaachilia mara moja na bila masharti waandishi wa habari waliokamatwa mjini Mbeya.

Kulingana na taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari na Jukwaa hilo, waandishi hao walikuwa wakisubiri kufanya mahojiano na viongozi wa Chadema waliokuwa wanaendelea na kikao cha ndani ofisini.

Taarifa hiyo imeongezea kwamba waandishi hao wanaotoka mjini Dar es salaam kwasasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mbalizi.

‘’Tunavisihi vyombo vya dola kuwaachia mara moja waandishi hao na bila masharti kwa sababu kuwapo kwao katika eneo la tukio, tunaamini walikuwa wanafanya kazi na si sehemu ya siasa au chochote kilichokuwa kinaendelea,’’ alisema taarifa iliotiwa sahihi na mwenyekiti wa jukwaa hilo bwana Deodatus Balile.

Vilevile Jukwaa hilo limelaani tukio hilo likisema linaharibu heshima kubwa ya Tanzania katika kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari aliyoujenga Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live