Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani kumrithi Kinana CCM?

Nani Kumrithi Kinana CCM Nani kumrithi Kinana CCM?

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nani mrithi wa nafasi ya makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara? Hili ndilo swali linaloulizwa na wengi baada ya aliyekuwa na wadhifa huo, Abdulrahman Kinana kujiuzulu.

Taarifa ya kujiuzulu kwa Kinana ilitolewa juzi na CCM, ikinukuu sehemu ya barua ya Rais Samia Suluhu Hassan, mwenyekiti wa chama hicho, akijibu “kukubali kwa moyo mzito” ombi la mwanasiasa huyo mkongwe.

Uamuzi wa Kinana umeibua kiu ya wadau wa siasa, makada na wafuasi wa chama hicho, kujua nani atakayerithi mikoba ya mwanasiasa huyo.

Shauku ya wadau hao inapozwa na taarifa za ndani ambazo Mwananchi linazo kuwa, miongoni mwa wanasiasa walio karibu kuirithi nafasi hiyo, ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.

Pinda ambaye ambaye tangu amestaafu uwaziri mkuu mwaka 2015 ameendelea kuwemo kwenye vikao vya juu ya CCM kwa njia ya uteuzi, na hadi sasa akiwa mjumbe wa Kamati Kuu, anatajwa kuwa mtu sahihi wa kuvaa viatu vya Kinana.

Hata hivyo, Pinda hakutajwa peke yake, pia wamo aliyewahi kuwa waziri kwa muda mrefu Steven Wasira, Waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye na mwenyekiti mstaafu wa Jumuiya ya Wazazi, Abdallah Bulembo, miongoni mwa wanaohusishwa na kurithi wadhifa huo wa pili kwa ukubwa ndani ya CCM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live