Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpina: Kamati ya Bunge iliongeza mashtaka tofauti na maelekezo ya Spika

Mheshimiwa Luhaga Mpina Mpina: Kamati ya Bunge iliongeza mashtaka tofauti na maelekezo ya Spika

Sun, 30 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina anayetumikia adhabu ya kutohudhuria Vikao 15 vya Bunge kutokana na Kudharau Kiti cha Spika na Bunge, amesema Kamati ya Haki na Madaraka ya Bunge iliongeza mashtaka tofauti na maelekezo ya Spika.

Amesema “Spika alisoma hadharani mashtaka yangu kuwa nimeenda kinyume na Kifungu cha 29 D na E na Kifungu cha 34(1) G cha Sheria na Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na siyo Kifungu cha 26 D na E na Kanuni ya 84(1) J na K, hawa Watu wa Kamati walivipata wapi wakati katika vifungu vya Spika hazikuwepo?”

Ameongeza vifungu vilivyoongezwa haviendani na maudhui ya tuhuma zilizotolewa na Spika, akisema kifungu hicho kinazungumzia makosa ya Waandishi wa Habari wanapoingia katika Vikao vya Bunge bila kufuata utaratibu na hakiendani na Kosa la Jinai wala kinidhamu kwake

Pia, amesema “Nilitegemea Spika angechukizwa na Waziri Bashe pamoja na Waziri Mwigulu kutokana na ushahidi uliopelekwa mbele yake, badala yake imekuwa kinyume chake.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live