Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkutano wa kumpata mrithi wa Mrema waota mbawa-VIDEO

MREMA MCHAKATO Mkutano wa kumpata mrithi wa Mrema waota mbawa

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkutano Mkuu uliokuwa ufanyike leo Marchi 6, 2023 ili pamoja na mambo mengine, kujaza nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema umeshindwa kufanyika baada ya kupokea barua kutoka kwa wadhamini wa chama.

Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lyimo, amesema wadhamini hao walishauri kusitisha kwa mkutano huo Mkuu kwa kuwa kabla ya mkutano huo, kuulitangulia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa jijini Dar ambacho wadhamini wa chama wamedai kulikuwa na mapungufu.

"Leo Machi 6, 2023 tulikuwa na mkutano mkuu wa kujaza nafasi za uongozi ziliyokuwa wazi ikiwemo ya Mwenyekiti Marehemu Agustino Mrema, wakati tunajiandaa tulipata barua kutoka kwa wadhamini wakisema mkutano huo usifanyike kutokana na kutokuwa na mazingira mazuri," Richard Lyimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: