Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makalla: Lissu akitaka gari mpya CCM tutamnunulia

Makalla 178096 Makalla: Lissu akitaka gari mpya CCM tutamnunulia

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa NEC- Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Amos Makalla amempongeza Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kwa kupokea Tsh. milioni 5.3 alizopewa na CCM kwa ajili ya kumchangia kurekebisha gari alilopigwa nalo risasi huku akisema hata kama akitaka gari jipya CCM itachanga na kumsaidia alipate.

Akiongea jana August 27,2024 akiwa kwenye ziara ya kusikiliza kero Wilayani Kigamboni Jijini Dar es salaam, Makalla amesema “Tumeanzisha harambee ya kumsaidia gari lake litengenezwe (Tundu Lissu), nawashukuru Wana CCM na Wana Mwanza kwa kukubali harambee ile tukapata Mil 5.3 nikamtumia Mtani wangu (Lissu) na yeye akanijibu asante sana na atatengeneza gari na Lissu sasa ataendelea na kazi zake piga makofi kwa Wana CCM.

“Kama matengenezo yatamsumbua sana hata akitaka jipya sisi tutachanga tutamsaidia Lissu na sisi tupo tayari hata akinitaka sasa Mtani wake nifanye harambee tutamchangia apate gari jipya Lissu ili aendelee na kazi, tutaendelea kuwasaidia na sisi tunathibitisha 4R za Mh. Rais, kusaidiana, kuvumiliana.

“Na Mimi nafurahi baada ya kuchanga CHADEMA wakasema ‘aah Lissu hawezi kupokea hela tutahakikisha tunazirudisha’ kwani CHADEMA nyie tuliwachangia!?, tumemchangia Lissu kama Lissu na nampongeza Lissu akasema nimepokea na nautambua mchango huu nimechangiwa kama Mtu yoyote hata wakati ule nilipopata matatizo nilichangiwa na Wana CCM na wasiokuwa Wana CCM”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live