Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lema: Naweza kuwalipa wabunge wanne mshahara, wamhudumie mke wangu-VIDEO

LEMAAA Lema: Naweza kuwalipa wabunge wanne mshahara, wamhudumie mke wangu

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amezidi kukazia kauli yake kuwa bodaboda sio kazi salama kwa vijana.

Lema amesema, yupo tayari kupoteza hata ubunge kama endapo hawatamchagua kwa kuwaeleza ukweli huo kwani yeye mshahara wa ubunge kwake sio kitu na anaweza kuwalipa wabunge wanne mshahara na akawapa kazi ya kumtetea mke wake.

"Siishi kwa ajili ya kuwa mbunge, naishi kwa ajili ya baraka ya kizazi kinachokuja. Ubunge, mimi ni mchaga, sipigani kuwa mbunge ili nipate mshahara wa milioni kumi, mshahara wa milioni kumi ni kidogo sana.

"Naweza kuwalipa wabunge wanne kila mwezi na nikawapa kazi moja tu ya kumtetea mke wangu pindi ninapochelewa kurudi nyumbani," alisema Lema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: