Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LHRC yatoa wito Chadema waachiwe

LHRC ANA HENGA LHRC yatoa wito Chadema waachiwe

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimelaani vikali hatua ya Jeshi la Polisi kuwashikilia baadhi ya Viongozi na Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadhi ya Waandishi wa Habari, hatua hii inakuja baada ya Chama hicho kupanga kufanya kongamano la maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani lililopangwa kufanyika leo August 12, 2024 Jijini Mbeya.

Taarifa iliyotolewa leo August 12,2024 na Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga imesema “Inadaiwa Viongozi na Wafuasi hao walikamatwa jana kwa nyakati tofauti wakati wakiwa katika maandalizi ya kongamano hilo na wengine wakiwa safarini kuelekea Mbeya, kwa mujibu wa ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, kifungu cha 11 cha Sheria ya Vyama vya Siasa sura Na. 258 na marekebisho yake ya mwaka 2024, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa mwaka 1966 na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu wa mwaka 1981, ni haki ya Vyama vya Siasa kufanya mikutano ya hadhara, makongamano pamoja na maandamano”

“Kitendo hiki pia kinapingana na msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye Januari 2023 alitangaza kufuta zuio la mikutano ya hadhara sanjali na shughuli nyinginezo za kisiasa ambazo zilikuwa zimepigwa marufuku tangu mwaka 2016, wakati huohuo hatua ya Polisi kuzuia shughuli halali za kisiasa inakwenda kinyume na dhana ya 4R za Rais zilizolenga kuleta maridhiano na ustahimilivu wa tofauti za kisiasa” —— Anna Henga.

“Tukio hili linaonekana kuwa na sura ya ubaguzi, kwani tumeshuhudia Vijana wa Vyama vingine wakifanya maadhimisho yao bila kikwazo chochote, kwa mfano, Vijana wa CCM walikusanyika Uwanja wa Amani, Zanzibar, August 10, 2024, na kufanya maadhimisho yao bila bughudha yoyote, hali kadhalika Vijana wa ACT Wazalendo walifanya maadhimisho yao August 11,2024 huko Wete, Pemba” ——— Anna Henga.

“LHRC inatoa wito kwa Polisi na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama Nchini kuwaachilia huru Viongozi na Wafuasi hao bila masharti yoyote ili waweze kutekeleza wajibu na haki za kufanya shughuli za kisiasa kwa mujibu wa sheria, LHRC inaendelea kufuatilia tukio hili kwa karibu na hatua zaidi” ——— Anna Henga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live