Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kambaya asema CHADEMA wamekiuka makubaliano, wamegawana majimbo

Chadema Mjk Kambaya asema CHADEMA wamekiuka makubaliano, wamegawana majimbo

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya viongozi wa waliokuwa wanachama 608 ambao walijiunga na chama cha CHADEMA kutoka chama cha wananchi CUF wametangaza kujiondoa Chadema kutokana na sababu mbalimbali.

Miongoni mwa sababu hizo ni kukosa ofisi. Malipo ya uanachama pamoja na masuala mengine ambayo wameshindwa kuyaweka wazi.

Viongozi hao wakiongozwa na Abdul Kambaya ambao walijiunga na CHADEMA miezi miwili iliyopita wakitoka cuf wametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza kwa niaba ya wenzakea Abdul Kambaya amesema baada ya kutoridhishwa na baadhi ya changamoto kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA  ambazo zimewafanya wajiondoe.

Wamesema wanatarajia kukaa nje ya siasa kwa muda ili kupumzika kabla ya kutafuta chama  kingine watakacho jiunga nacho.

Kwa upande wake Ismail Rajabu Nyota aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya kuwahamisha wanachama hao kutoka  CUF  kwenda CHADEMA amesema licha wao kuondoka pia wenzao nao wapo mbioni kuondoka CHADEMA kutokana na kutoridhishwa na mambo mbalimbali ikiwemo CHADEMA kukiuka makubaliano waliyokubaliana wakati wanajiunga na chama hicho.

Naye Shuga Simba na Shabani Mbugi wamesema licha ya kujivua uanachama wa Chadema hawana tatizo na  mwenyekiti wa CHADEMA ila changamoto ni watendaji wa chini wa Mbowe ambao walikiuka makubaliano waliojiwekea na hivyo kuwafanya kujiengua.

Wananchama waliojiengua leo ni 10 kati ya 600 ambao walijiunga miezi miwili iliyopita na kupokelewa na  Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe wakitoka CUF kabla ya leo kutangaza kujiondoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: