Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JK atoboa siri ya mafanikio CCM

JK Kikwete 696x461 JK atoboa siri ya mafanikio CCM

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete amesema anafurahishwa na namna makada, wanachama na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya uongozi wa Rais wa Samia Suluhu Hassan, wanavyoendeleza umoja miongoni mwao.

Mwenyekiti huyo Mstaafu wa CCM amesema umoja miongoni mwa wanachama ndio imekuwa nguzo na silaha muhimu hasa wakati huu wa kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwakani na ndio umekuwa ukikiletea chama hicho mafanikio.

Kiongozi huyo mstaafu amesema hayo Jijini Dar es Salaam alipofanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi aliyemtembelea kumjulia hali kwenye ofisi yake binafsi.

Kikwete ametumia nafasi hiyo kumwambia Balozi Nchimbi kuwa anafurahishwa pia na maelekezo anayotoa Mwenyekiti wa CCM, Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwataka viongozi wa chama kushuka chini kwa wanachama na wananchi ili kuwasikiliza na kutatua kero zao na kwamba anashukuru kuona hilo likifanyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live