Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halima Mdee: Kuwahamisha tu haitoshi, tengueni nafasi zao

Halima Mdee Bungeni Halima Mdee

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Halima Mdee jana amewasilisha Bungeni taarifa ya Kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge yaliyotokana na taarifa ya CAG kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ambapo amesema Serikali imekiuka maazimio ya Bunge ya kuwaondoa katika nafasi zao Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Ugavi 23 waliobainika kuwa na utendaji usioridhisha kwa kuwapangia majukumu mengine badala ya kuwawajibisha.

“Kumekuwa na ukiukwaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Sura 410 na Kanuni zake kwa baadhi ya Maafisa Masuuli katika Halmashauri mbalimbali nchini, lengo la Azimio lilikuwa ni kuhakikisha watendaji wote waliohusika na upotevu wa fedha za Umma kulikosababishwa na kukiukwa kwa matakwa ya Sheria hiyo kuchukuliwa hatua stahiki”

“Hata hivyo, Kamati imesikitishwa na hatua iliyochukuliwa na Serikali kwa kukiuka maazimio yaliyotolewa na Bunge kwa kuwaondoa katika nafasi zao Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Ugavi 23 waliobainika kuwa na utendaji usioridhisha na kusababisha hasara kwa kuwapangia majukumu mengine badala ya kuwawajibisha na kulipia hasara waliyoisababisha kama ilivyoainishwa na Kanuni ya 53 ya Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298, kwakuwa kuwaondoa pekee ni kuzidi kuiongezea mzigo Serikali (wage bill) kwakuwa watalipwa mishahara yao kama ambavyo walivyokuwa katika nafasi zao za awali”

“Katika hoja hiyohiyo, Serikali imeeleza kuwabadilisha vituo vya kazi Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi na Ugavi 68 kinyume na Azimio la Bunge la kuwachukulia hatua kali za kisheria, tafsiri ya haraka na maoni ya Kamati kuhusu hoja hii ni kuhamisha tatizo kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine ikiwa ni pamoja na kuwaaminisha Watumishi hao kuwa, hakuna hatua zozote za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yao pindi watakapokiuka taratibu za kiutendaji”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: