Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yawang'oa viongozi wawili - VIDEO

Video Archive
Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati Kuu Maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan iliyokutana leo Jumapili, Septemba 1, 2024 pamoja na mambo mengine imewavua madaraka viongozi wake wawili akiwemo wa Jumuiya ya Wanawake (UWT).

Chama hicho kimemuondoa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Lindi, Palina Ninje pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Abdul Zahoro.

Uamuzi huo umetangazwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla wakati akizungumza na waandishi wa habari akitoa mrejesho wa yaliyozungumzwa kwenye kikao cha kamati hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live