Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yatoa neno kufunguiwa kwa muda Ziwa Tanganyika

Makala CCM yatoa neno kufunguiwa kwa muda Ziwa Tanganyika

Mon, 5 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema chanzo cha Ziwa Tanganyika kufungwa kwa muda ni kuongeza mazalia ya samaki na si kuwanyanyasa wananchi kama baadhi ya wanasiasa wanavyodai.

Makala amesema hayo jana Jumapili Agosti 4, 2024 katika ziara ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi mkoani Kigoma.

“Wapo wanasiasa walikuja wakasema maneno ya uchochezi kwamba Serikali ya CCM inanyanyasa wavuvi, nataka niseme neno… duniani kote zinatungwa sheria na kanuni kwamba samaki au mazao ya baharini au ziwa yanapopungua, wadau wanakaa wanakubaliana kwamba tuongeze mazalia ya samaki, hapa Ziwa Tanganyika dagaa walipungua na wakakubaliana kulifunga kwa muda,” amesema Makalla.

Ziwa hilo lilifungwa Mei 15, 2024 na linatarajiwa kufunguliwa Agosti 15, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live