Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yamchangia Lissu sh milioni 5 atengeneze gari lake

Lissu Nchimbi CCM yamchangia Lissu sh milioni 5 atengeneze gari lake

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza wamejitolea kumchangia Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu Sh milioni 5.3 kwa ajili ya kutengeneza gari lake.

Harambee ya kumchangia Lissu atengeneze gari lake imefanyika katika Mkutano wa Hadhara Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi aliwashukuru wanaCCM wa kawaida kutoa kwa michango kumsaidia Lissu atengeneze gari lake ambalo ni bovu baada viongozi wa CCM kuguswa na tatizo la gari la Lissu.

"Lissu ana haki ya kuishi kama wengine, asibanwe atengeneze gari lake," alisema Dk Nchimbi.

Dk Nchimbi alisema amefurahi jambo walilofanya wana-CCM kumchangia Lissu kutengeneza gari ndivyo 4R za Rais Samia hazitaki watu wapambane bali zinataka watu wapendane na kusaidiana.

Akawashukuru wana CCM wa Mwanza kwa kuguswa kumsaidia Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara Wakili Tundu Lissu ambaye anatembelea gari bovu na walinzi wake 15 ili atengeneze.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live