Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM Mbeya yatoa mwezi mmoja ujenzi mfereji makaburi ya Isanga

CCM Mbeya Yatoa Mwezi Mmoja Ujenzi Mfereji Makaburi Ya Isanga CCM Mbeya yatoa mwezi mmoja ujenzi mfereji makaburi ya Isanga

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CCM Mbeya yatoa mwezi mmoja ujenzi mfereji makaburi ya Isanga Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeingilia kati na kutoa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kujenga miundombinu ya mfereji katika makaburi ya Isanga Mtaa wa mkuyuni Kata ya Iganzo.

Hatua hiyo imetokana na malalamiko ya wananchi baada ya makaburi kufukuliwa na maji kipindi cha mvua na miili kuelea juu hali inayozua taharuki kwa wananchi. Hali hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara kunapokuwa na mvua nyingi.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Juni 12,2024 Katibu Mwenezi CCM mkoani Iringa, Christopher Uhagile amesema ni jambo la fedheha kwa jiji kushindwa kuboresha miundombinu hiyo na kusababisha miili kuonekana hadharani jambo ambalo sio la kawaida.

"Nimezungumza na Diwani wa Kata ya Iganzo amenipa picha halisi ya eneo hilo la makaburi na kadhia ambayo wananchi wanakumbana nayo mvua zinaponyesha.”

“Si sawa watu kuona miili ya watu waliopoteza maisha ikielea au kusombwa na maji"amesema Uhagile.

Amesema kama chama watekelezaji wa ilani hawataweza kuvumilia jamii kuendelea kulalamikia suala hilo ambalo limeripotiwa miaka mitatu iliyopita pasipo kulifanyiwa maamuzi.

"Kuanzia sasa ndani ya siku 30 tutafuatilia kuona kama Serikali imetekeleza ujenzi wa mfereji ili kurejesha amani na utulivu kwa jamii inayoishi jirani na makaburi hayo,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live