Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT Wazalendo yafungua kesi kupinga TAMISEMI kusimamia uchaguzi

Sitakuwa Kama Zitto Kabwe   Semu Dorothy Semu.

Mon, 26 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akihutubia katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya #ACTWazalendo, Kiongozi wa Chama, Dorothy Semu amesema Chama Tawala (CCM) na Serikali yake kimeanza kuonesha hila zao kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Amesema "Wameanza kuminya #Uhuru wa Vyama na Wananachama. Wameanza vitisho, ubabe na kutosikilizana."

Aidha, Dorothy amesema Chama cha ACT Wazalendo kimeshapeleka kesi Mahakamani kuzuia #TAMISEMI, kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Taifa la wote, Maslahi kwa wote! Zanzibar Mpya, Zanzibar Moja Mamlaka kamili.

Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasihii adhimu ya kukutana nanyi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya kwanza tangu chama chetu kipateuongozi mpya baada ya Uchaguzi Mkuu Machi mwaka2024.

Kwa heshima kubwa, napenda kuwakaribishakatika kikao hiki muhimu.

Ndugu wajumbe wa Halmashauri Kuu, tarehe 27 Mei, 2024 nilipozungumza na wanachama, viongozi na taifakwa ujumla kule Moshi, Kilimanjaro katika maadhimishoya miaka 10 ya chama chetu niliwaeleza juu ya hali mbayatuliyopitia na tuliyonayo katika nchi yetu.

Niliwaeleza hali ya mwenendo wa uchumi wa nchi hasaukubwa wa deni la Serikali na athari zake kwa wananchi walalahoi, tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wetu, halingumu ya maisha, kilio cha wazee wastaafu kuhusukikotoo cha mafao na huduma mbovu za afya na gharamakubwa za matibabu.

Julai 22 hadi Agosti 17 tulipokuwa kwenye ziara katikaMikoa 22 na majimbo 125 tumekutana na mambo yale yale. Sasa sitaki kuyarudia hayo lakini kuna masuala kadhaa ni muhimu kuyasisitiza tena kwa namna mambo yanavyoendelea nchini na umuhimu wa kikao hiki ambacho wajumbe wake wanatoka maeneo mbalimbali yanchi yetu.

Hivyo, kuna mambo yanayoendelea nchini yanapaswakujadiliwa, kutazamwa na kueleweka na kila mmoja wetuhasa sisi viongozi.

Migogoro ya Ardhi Kuna mwanazuoni maarufu nchini katika kuelezea jamboaliandika kwamba “Utalii unatuangamiza. Uhifadhi kiholela bila kujali maslahiya waishio karibu na eneo husika unazaa migogoro. Hatima yake ni mateso na ukatili kwa wananchi kutokanana vyombo vya mabavu ya Serikali kutodhibitiwa nakutowajibishwa. Chanzo cha migogoro mingi ya ardhinchini ni serikali yenyewe. Ukatili na mateso hayatakomakama jamii itakaa kimya. Uvumilivu una mwisho! Utulivubila haki ni feki. Unasubiri kulipuka.” Issa Shivj, Mei 9, 2024.

Hii ni mara ya pili Halmashauri kuu hii tunalileta suala la ardhi. Wimbi la uporaji na migogoro ya ardhi ni kubwa naimekuwa tishio kwa amani na utulivu wa nchi yetu. Uchambuzi wetu unaonyesha kuwa migogoro hii ipomakundi makuu matatu.

Migogoro ya mipaka kati ya vijiji na mamlaka za hifadhi (TANAPA, TFS,TAWA) Tatizo la migogoro ya mipaka imekuwa na athari kubwakwa wananchi ikiwemo kunyang’anywa mifugo, mazao, vitisho, vipigo na vifo vya watu (wananchi na askari wauhifadhi). Kwa mujibu wa taarifa za Serikali Vijijivinavyoainishwa kuwepo katika migogoro hiyo ni vijiji 975 ambavyo vinapakana na mamlaka za hifadhi kuanziahifadhi za taifa, hifadhi ya Ngorongoro, mapori tengefu namapori ya akiba. Mifano ya maeneo yenye migogoro hiyoni Mbarali, Ngorongoro, Kasulu, Uvinza, Loliondo, Kaliua na Kilwa.

Mtakumbuka hali ilivyo sasa huko Ngorongoro. Takribaninusu karne wananchi jamii ya kimasai katika Tarafa yaNgorongoro na Loliondo wamekuwa wakiishi katikamashaka kwenye ardhi zao. Tishio kubwa zaidi limeibukahivi karibuni kwa Serikali kuwaondoa kabisa wamasaikatika ardhi hiyo (Kuwahamishia Msomera), kufanyaoperesheni inayoambatana na mateso, kuzuia huduma za kijamii, kuondoa majina yao kwenye daftari la wapiga kurana jaribio la kufuta vijiji 25 na vitongoji 96.

Viongozi wenu kupitia Baraza Kivuli la Mawaziri tumekuwamstari wa mbele kusimama na wananchi wa Ngorongoro na maeneo mengine kulinda haki ya ardhi kwa wananchi. Tunaendelea kuitaka Serikali kuruhusu haki ya ardhi kwawananchi wa Ngorongoro kama ilivyo kwa Watanzaniawengine. Pia, tunaitaka ibatilishe tangazo haramu na 673 la 2024 linalotaka kufuta vijiji vya Ngorongoro na maeneomengine nchini. Itekeleza haraka kurejesha majina yaliyondolewa kwenye daftari la wapiga kura.

Aidha, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ivunjwe na iundweKampuni yenye ushiriki na umiliki wa ubia kati ya Serikalina wananchi wa Ngorongoro kumaliza mgogoro.

Wito wangu kwenu, tusiyumbishwe na propanda za Serikali inayojielekeza kuwashambulia wananchi kwakuwaita wavamizi na majina mengine. Suala la migogoroya ardhi linapaswa kupewa uzito mkubwa katika mijadalaya kisera.

Tunaamini katika TAIFA LA WOTE, MASLAHI YA WOTE. Hivyo ardhi lazima iwe na manufaa kwa wotena sio Serikali au wawekezaji tu.

Matukio ya utekaji na matishio ya usalama Hivi karibuni kumeibuka tena kwa kasi matukio ya utekaji, kupotea na mauaji ya raia hasa wananchi wanaonekanakuikosoa Serikali au wanaohoji matukio yasiyofaa kuhusuviongozi wa Serikali. Chama cha wanasheria Tanganyika kilitoa orodha ya watu zaidi ya 89 waliopatwa na madhilahayo.

Watanzania wameanza kuingiwa tena na hofu kukithirikwa matukio haya. Inasikitisha zaidi kuona watu wakwanza wanaohusishwa na matukio haya ni Jeshi la Polisi na baadhi ya matukio wananchi wanalalamikia Polisi kutochukua hatua za haraka kwa wanaohusika na matukiohayo.

Chama cha ACT Wazalendo, tunalaani kwa nguvu zotekuongezeka kwa matukio hayo bila hatua madhubutikuchukuliwa. Ni wakati wa kusukuma madai ya mageuziya Jeshi la Polisi hasa kutoruhusu kutumika kisiasa. Jeshila Polisi linapaswa kujiendesha kwa weledi.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa OR- TAMISEMI imetangaza uchaguzi wa Serikali za Mitaautakaofanyika Novemba mwaka 2024. Chama tumejiandaa vyema kushiriki na leo itakuwa ajenda kubwa, tutajadiliana namna tunavyopaswa kujiandaa, kujipangana kuhakikisha uchaguzi huu unatuweka katika nafasinzuri ya ushindi.

Chama Tawala na Serikali yake kimenza kuonesha hila zao kuelekea kwenye uchaguzi huo, wameanza kubinyauhuru wa vyama na wananchama. Wameanza vitisho, ubabe na kutosikilizana. Tumeshapeleka kesimahakamani kuzuia TAMISEMI wizara ya Serikalikusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Hitimisho Hali hii ya kiuchumi inatuonesha kuwa bado mapambanoyetu ya kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika nazinalitufaifa taifa letu (kwa maslahi ya wote na siowachache wale wale) yanapaswa kuendelea nakuongezewa nguvu mara dafu sasa kuliko wakatimwingine katika historia ya chama chetu.

Chama cha ACT-Wazalendo kinapaswa kuongoza umma kwa ajili ya kufufua matumaini ya wananchi waliokatatamaa ili kila Mtanzania aone kuwa atanufaika na utajiriwa taifa letu. Ni wajibu wetu kuongoza wananchi kuonawana wajibu wa kujenga nchi yao ili kulinda na kudumishausawa, ustawi wa jamii, uwajibikaji, demokrasia, nauongozi bora.

Ndugu Wajumbe, katika kumaliza hotuba yangu napendakuwajulisha rasmi kuwa mapema mwezi ujao tutafanyaziara ya awamu ya pili ya kufikia majimbo ambayoyamebakia baada ya ziara ya awamu ya kwanza. Baadaya ziara hiyo tutakuwa tumeyafikia majimbo yote 214 yaTanzania bara. Kwa upande wa Zanzibar ziara ya kufikiamajimbo yote 50 inaendelea. Nawaomba viongozimjiandae vizuri na ziara hizi ili tuweze kupata mafanikio yanayotakiwa na kukifanya chama chetu kuwa sauti yawananchi wetu. Chama cha siasa ni watu, ni wajibu wetukuwa watetezi wa watu wetu.

Nawatakia kila la kheri katika mkutano huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live