Nchi

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuNchiPeopleIndustry
Reginald Abraham Mengi

Watu Maarufu Tanzania

Industry

Reginald Abraham Mengi

Mfahamu Reginald Mengi

Mengii
Tarehe ya Kuzaliwa:
1942-05-29
Mahali pa Kuzaliwa:
Machame, Kilimanjaro
Date of Death:
2019-05-02
DECEASED

Reginald Mengi ni jina kubwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, lakini wajua ametokea wapi. Mengi alizaliwa wilayani Machame, Kilimanjaro, Tanzania mwaka 29 Mei 1942, akiwa mmoja wa watoto saba wa Bw Abhraham Mengi na Bi Ndeekyo Mengi.

Alianza safari yake kielimu shule katika shule ya msingi Kisereny Village Bush School, kisha akajiunga Nkuu District School, kisha Siha Middle School, na baadaye Old Moshi Secondary School. Kwa ufadhili wa Chama cha Ushirika kilichokuwa na nguvu ya kifedha ushawishi KNCU Mengi alisomeshwa masomo yake ya shahada ya kwanza ya uhasibu nchini Uingereza.

Baada ya masomo ughaibuni, Mengi alirudi Tanzania 1971 na kuajiriwa na kampuni ya Cooper and Lybrand Tanzania ( sasa Prince water house Cooper) mpaka mwaka 1989 alipoamua kujikita kwenye ujasiriamali.

Ujasiriamali na kufanikiwa

Baada ya kuachana na ajira, Mengi aliiboresha kampuni yake ya Industrial Projects Promotion Limited na baadae kufahamika zaidi kama IPP Limited.

Kupitia IPP Limited Mengi alianzisha kampuni mbalimbali na kufanya biashara kadha wa kadha kuanzia uzalishaji wa sabuni, soda, maji ya kunywa, madini, mafuta, gesi asilia na kilimo.

Hata hivyo, umaarufu mkubwa wa Mengi ni kutokana na kumiliki vyombo vya habari, kuanzia magazeti, vituo vya runinga na redio. Runinga yake ya ITV pamoja na kituo cha Redio One ni moja ya vituo vikubwa vya utangazaji huku magazeti yake ya Guardian na Nipashe yakiwa miongoni mwa magazeti makubwa zaidi Tanzania.

"Nimezaliwa katika umasikini wa kutupwa, lakini jambo hilo hata siku moja halikunikatisha tamaa," ni moja ya kauli ambazo Reginald Abraham Mengi alikuwa hacoki kuzisema kila alipopata wasaa wa kuzungumzia alipotokea maishani.

Ni jambo hilo pia ndilo lilomsukuma kuchapisha kitabu cha maisha yake mwaka 2018 kiitwacho I can, I must, I will (Ninaweza, Lazima nifanye, Nitafanikisha) kinachoangazia historia ya maisha yake toka alipozaliwa mpaka kufanikiwa kibiashara

Mzee Mengi alifariki Jumatano usiku 2 Mei 2019, jijini Dubai, Falme za Kiarabu alipokwenda kwa matibabu.

Mpaka umauti unamfika, alikuwa mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Tanzania.

Mengi pia amekuwa akijitoa katika kusaidia wasionacho na wenye uhitaji kwenye jamii ikiwemo walemavu wa ngozi na kugharamia matibabu ya watoto wnye matatizo ya moyo nchini India.

Mwaka 2014, jarida maarufu la masuala ya fedha Forbes lilikadiria utajiri wa Mengi kuwa unafikia dola milioni 560.

BBC