Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Verstappen ashinda mbio za 8 za Langa langa 2022

Max  Verstappen Verstappen dereva wa kampuni ya magari ya Red Bull

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Max Verstappen dereva wa kampuni ya magari ya Red Bull ameshinda mbio za Hangari Grand Prix.

Huu ni ushindi wa 8 msimu huu kwa Max kwenye mbio 13 zilizofanyika msimu huu wa 2022 kwenye Langa Langa.

Kwa ushindi huu wa Leo dereva huyo raia wa Uholanzi amefikisha alama 258 akiwa ndio kinara kwenye msimamo wa madereva na anaongoza kwa tofauti ya alama 80 dhidi ya Charles Leclerc dereva wa Ferrari aliyenafasi ya pili akiwa na alama 178.

Kwenye mbio hizo za Hangarian GP nafasi ya pili na ya tatu wameshika madereva kutoka Mercedes Lewis Hamilton nafasi ya pili na nafasi ya tatu imeenda kwa George Russell. Ni mbio za 5 mfululizo Hamilton anamaliza kwenye nafasi 3 za juu msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live