Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Verstappen alivyonufaika na changamoto za Leclerc

57973810 303 Max Verstappen akishangilia ushindi

Tue, 24 May 2022 Chanzo: eatv.tv

Charles Leclerc wa Ferrari alikuwa kwenye nafasi ya kuongeza wigo wa alama dhidi ya wapinzani wake kwenye mashindano ya Spanish Grand Prix lakini akashindwa kufuatia injini ya gari lake kupata hitilafuna kumpa nafasi mpinzani wake Max Verstappen kupunguza tofauti baina yao.

Haikuwa raishi kwa Verstappen, ambaye alistahimili kwenye mzunguko ya kwenye barabara ya changarawe huku akikumbana na vikwazo kwa takribani mizunguko 20 wakiwa nyuma ya Mercedes ya George Russell kabla yeye na timu yake ya Red Bull kufanikiwa kurudi katika uongozi.

Kukwamba kwa Leclerc imekuwa manufaa kwa Verstappen ambaye sasaa ina uongozi wa pointi sita kileleni mwa msimamo na anaongoza kwa mara ya kwanza msimu huu na si hivyo tu, lakini takwimu zinaonekana kuwa mbaya kwa Leclerc na timu yake ya Ferrari.

Huu ulikuwa ushindi wa tatu mfululizo kwa Verstappen ingawa kabla ya kuona wanafanikiwa swali kuu ni je ataweza kuendeleza ushindi dhidi ya juu ya Red Bull.

Baada ya kuanza kwa msimu kwa shida kwa gari lililokuwa na hitilafu, ghafla Russell na Lewis Hamilton walionekana kana kwamba wanaweza kuanza kufanya maisha kuwa magumu kwa Verstappen na Leclerc hivyo huenda mashindano ya msimu huu yakawa na matokeo ya kushangaza.

Chanzo: eatv.tv