Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Timu ya Rugby ya Afrika Kusini yafanikiwa kutinga fainali ya kombe la dunia

Timu Ya Rugby Ya Afrika Kusini Yafanikiwa Kutinga Fainali Ya Kombe La Dunia Timu ya Rugby ya Afrika Kusini yafanikiwa kutinga fainali ya kombe la dunia

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: Voa

Timu ya taifa ya Rugby ya Afrika Kusini imefanikiwa kuingia fainali ya michuano hiyo ya kombe la dunia baada ya kuishinda Uingereza kwa pointi 16-15 katika mchezo mkali na kusisimua ambao Uingereza walitawala kwa sehemu kubwa.

Timu ya taifa ya Rugby ya Afrika Kusini imefanikiwa kuingia fainali ya michuano hiyo ya kombe la dunia baada ya kuishinda Uingereza kwa pointi 16-15 katika mchezo mkali na kusisimua ambao Uingereza walitawala kwa sehemu kubwa.

Nahodha Siya Kolisi na kocha Jacques Nienaber walisema mabingwa hao watetezi walilazimika kutumia nguvu zao zote ili kupata ushindi wao finyu wakitokea nyuma katika uwanja wa Stade de France ili kujikatia tiketi ya kucheza fainali wikendi ijayo dhidi ya timu ya New Zealand.

Ilikuwa ngumu sana leo, lakini kazi ngumu tuliyofanya imezaa matunda na ndivyo mabingwa wanavyofanya," Kolisi alisema wakati wa kusherehekea ushinmdi mwishoni mwa mchezo huo.

Flyhalf Handre Pollard, ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Mannie Libbok wakati Afrika Kusini ilipokuwa ikishambuliwa sana katika kipindi cha kwanza alipiga shuti la mbali na kuipatia ushini Springboks katika mechi hiyo.

Chanzo: Voa