Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Tanzania yavuna dhahabu ya kwanza riadha Afrika

Medali Pic Data Tanzania yavuna dhahabu ya kwanza riadha Afrika

Sat, 28 May 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mwanariadha Emmy Hosea amekuwa Mtanzania wa kwanza kutwaa medali kwenye mashindano ya vijana ya Afrika ya kanda yanayoendelea kwenye uwanja wa Mkapa.

Emmy ametwaa dhahabu hiyo kwenye mbio za mita 200 akitumiw sekunde 25.29 na kumuacha Mkenya, Silvier Chelengat aliyetumia sekunde 25.45.

Siwema Julius wa Tanzania aliyekimbia kwa sekunde 25. 91 alihitimisha tatu bora.

Hiyo ni medali ya kwanza ya dhahabu kwa Tanzania tangu kuanza kwa mashindano hayo jana Ijumaa.

"Maandalizi yetu yamechelewa, mpaka jana tulikuwa tumepata medali kama nane za fedha na shaba, leo tumepata medali ya kwanza ya dhahabu," amesema kocha mkuu wa timu hiyo, Yohana Misese.

Timu za Ethiopia, Kenya na Zanzibar zimegawana medali za dhahabu mpaka sasa kwenye mashindano hayo yanayotarajiwa kufungwa leo jioni.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz