Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Tanzania ya tatu Riadha Afrika

Riadha Pic Tanzania ya tatu Riadha Afrika

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania imemaliza kwenye nafasi ya tatu katika matokeo ya jumla kwa vijana chini ya miaka 20 mashindano ya riadha Afrika ya kanda.

Mashindano hayo ya siku mbili yamefungwa jana jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Ethiopia imetawazwa kuwa mabingwa wa jumla baada ya kuvuna medali sita, tano za dhahabu na fedha moja.

Kenya imetwaa nafasi ya pili ikiwa na medali 11, dhahabu nne, fedha tano na shaba mbili na Tanzania iliyovuna dhahabu moja, fedha tatu na shaba nne ikihitimisha tatu bora kwa wanariadha chini ya miaka 20.

Kwa wanariadha chini ya miaka 18, Ethiopia tena imeibuka vinara ikitwaa dhahabu 10, fedha tatu na shaba mbili.

Zanzibar imekamata nafasi ya pili ikiwa na dhahabu tatu, fedha tatu na shana nne huku Kenya ikihitimisha tatu bora ikiwa na dhahabu moja, fedha nne na shaba moja.

Kwa vijana wa umri huo, Tanzania imemaliza kwenye nafasi ya tano ikiwa na shaba tano na fedha moja nyuma ya Eritrea iliyomaliza ya nne.

Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Silas Isangi amesema bado wana nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika na dunia kwa vijana baadae mwaka huu.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Yohana Misese amesema matokeo hayo ni matunda ya walichopanda kwenye maandalizi.

"Tulichelewa kufanya maandalizi, lakini vijana wamepambana na tuitumie hii kama funzo kwenye mashindano yajayo," amesema Misese.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live