Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Tallis bingwa michuano ya Taifa ya kuogelea

Tallis Bingwa Michuano Ya Taifa Ya Kuogelea Tallis bingwa michuano ya Taifa ya kuogelea

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Tallis IST imetawazwa bingwa wa jumla wa Mashindano ya Klabu Bingwa Taifa yaliyomalizika jana kwenye Bwawa la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Masaki Dar es Salaam.

Tallis imeibuka Mabingwa katika mashindano hayo baada ya kujikusanyia pointi 385 huku Dar Swimming ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 330 na Mwanza akimalizia nafasi ya tatu akiwa na pointí 96.

Matokeo mengine ya timu za wanawake Taliss imejikusanyia pointi 241 wakifuatiwa na Dar Swimming mwenye pointi 84 na Ripted wakiwa na pointí 53.

Kwa upande wa wanaume Dar swimming imeng'ara kwa kujikusanyia pointi 236, huku Tallis IST 102 na Bandari 84.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha kuogelea Tanzania (TSA) Amina Mfaume amesema: "Namshukuru Mungu mashindano yameisha salama na washindi wamepatikana na watoto wameweza kuvunja rekodi ambayo ni mafanikio katika mchezo wa kuogelea ," - Amesema kuwa Kamati ya Ufundi itakutana kuangalia matokeo na kuchagua timu itakayoajiandaa kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa yakiwamo ya Mashindano ya Afrika Kanda ya tatu (CANA ZONE 3) na Dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live