Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Simbu: Tutapambana kuipa heshima Tanzania

Simbu Leo Common Alphonce Simbu

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha wa Tanzania, Alphonce Simbu, amesema amejipanga kuhakikisha anaipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki inayoendelea katika jiji la Paris, nchini Ufaransa.

Simbu na wanariadha wengine watatu, Gabriel Geay, Jacqline Sakilu na Magdalena Shauri, waliondoka nchini juzi kuelekea kwenye michezo hiyo.

Simbu, ambaye atakimbia kesho pamoja na Geay, alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri ili kupambania medali.

"Tunaomba Watanzania waendelee kutuombea, tutajituma na kupambana, binafsi nimejiandaa vizuri ili kuhakikisha ninaitangaza Tanzania katika riadha," alisema Simbu.

Wakati Simbu na Geay wakitarajiwa kukimbia kesho, wanaridha wa kike, Magdalena na Jacqline wenyewe watakimbia Agosti 11 kwenye kilele cha michezo hiyo.

Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Jackson Ndaweka amemuomba Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Ali Mwadini kuongoza Watanzania waishio nchini humo kujitokeza kwa wingi kuwashangilia wanariadha hao.

Ndaweka, alitoa ombi hilo juzi asubuhi wakati alipomtembelea na kupeleka taarifa ya ushiriki wa nchi ya Tanzania katika mashindano hayo kupitia mchezo wa riadha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live