Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Simbu, Geay kulipwa mamilioni maandalizi ya Olimpiki

Alphonceee Simbuu Simbu, Geay kulipwa mamilioni maandalizi ya Olimpiki

Fri, 17 Jun 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kitengo cha misaada (Olympic Solidarity) cha Kamati ya Olimpiki ya kimataifa (IOC) kimetoa 'scholarship' kwa wanamichezo watano nchini kwa ajili ya mazoezi ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki 2024 nchini Ufaransa.

Wanamichezo hao kila mmoja atakuwa akilipwa dola 1500 kwa mwezi ambayo itaanza kutolewa Julai mwaka huu hadi Agosti 2024.

Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi amesema ofa hiyo itatoa dola 40500 ambayo ni zaidi ya Sh 90 milioni kwa kila mchezaji kati ya watano waliopata 'scholarship' hiyo akiwamo Gabriel Geay na Alphonce Simbu.

Pesa hiyo itakuwa ikitolewa kila baada ya miezi minne ambapo mchezaji atakuwa akisaini dola 6000 ambayo ni zaidi ya Sh 12 milioni.

"Tanzania tuliwaombea wachezaji 16, lakini kulinganq na vigezo vya Olympic Solidary ni watano pekee ambao wamepata," amesema Bayi.

Amewataja wanamichezo wengine kuwa ni Failuna Abdi upande wa riadha, muogeleaji Hilal Hilal na mwanajudo, Thomas Mlugu.

"Hii scholarship ina masharti, miongoni mwake ni kama mcheza hautafuzu Olimpiki, atabadili uraia na utovu wa nidhamu inasitishwa," amesema.

Amesema lengo lake ni kuwaanda wanamichezo kwa ajili ya mafunzo ya mazoezi ya Olimpiki na kwa Tanzania zilianza mwaka 1999 kwa ajili ya Olimpiki ya 2000 na Michael Manino na Marko Hhawu walifikia vigezo vya kupata.

"Ni utaratibu ambao hufanyika kila baada ya miaka minne lakini kwa kuzingatia vigezo," alisema.

Katika utararibu huo Kamati ya Olimpiki Afrika (Anoca) pia inatoa ofa hizo, ambazo Bayi amesema vigezo vyake ni vigumu kushinda vile vya IOC.

"Anoca inatoa kwa mchezaji aliyetoka kushinda medali kwenye Olimpiki, awe kwenye 10 bora ya dunia kwenye michezo inayohusisha Olimpiki, vigezo ambavyo kwetu ni ngumu kupata ofa hiyo,".

Amewashauri wanariadha waliopata ofa hiyo kutumia pesa hizo ipasavyo ikiwamo kuwalipa makocha wao ili kufanya maandalizi stahiki kama ambavyo masharti ya scholarship hiyo yanataka.

Chanzo: Mwanaspoti