Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Rais Samia awapongeza Ramadhani Brothers

Ramadhani Brothers 5.jpeg Rais Samia awapongeza Ramadhani Brothers

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amewapongeza wanasarakasi Fadhili na Ibrahim maarufu kama The Ramadhani Brothers kwa kumaliza nafasi ya tano katika shindano la kusaka vipaji la American Got Talent (AGT) lilofanyika nchini Marekani.

“Hongereni sana Fadhili & Ibrahim (The Ramadhani Brothers) kwa hatua kubwa katika mashindano ya AGT 2023. Safari yenu ni alama ya Utanzania (bidii, nidhamu, kujituma, kujiamini na nia ya kufanya mambo makubwa). Mmeitangaza vyema nchi yetu. Mmelitendea vyema jina la Taifa letu,” ameandika Rais Samia.

Kundi hilo lilionesha mitindo yao ya sarakasi mbele ya majaji wanne akiwemo Simon Cowell, Sofia Vergara, Heidi Klum na Howie Mandel ambapo Adrian Stoica ndiye aliyeibuka mshindi wa AGT 2023.

Katika ukurasa wao wa Instagram, Ramadhani Brothers wameandika "Hatujapata kura za kutosha, tumekuwa watano katika shindano, na tunashukuru AGT kwa nafasi hii na watu wote waliotupigia kura, mapambano yanaendelea."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live