Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Rais ANOCA apokea kitabu cha Filbert Bayi, ampongeza

Olimpiki Pic Data Rais ANOCA apokea kitabu cha Filbert Bayi, ampongeza

Wed, 16 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Rais wa Kamati za Olimpiki Afrika (ANOCA), Mustapha Berraf amemuelezea nguli wa riadha nchini, Filbert Bayi kuwa miongoni mwa wanamichezo walioweka rekodi ya pekee.

Berraf amesema hayo jana wakati akipokea kitabu cha mwanariadha huyo nyota wa zamani kilichozinduliwa nchini Uingereza wiki kadhaa zilizopita chenye histori ya maisha yake kutoka kijijini hadi kuwa bingwa wa dunia wa mbio za mita 1500, kitabu kinachouzwa kwenye maduka ya Amazon duniani.

Akiwa kwenye mkutano wa makatibu wakuu wa kamati za Olimpiki Afrika, uliofanyika nchini Sierra Leone hivi karibuni, mwanariadha huyo nyota wa zamani nchini alimkabidhi Berraf kitabu hicho kijulikanacho kama "Catch Me If You Can".

Berrf alimpongeza Bayi na kubainisha kwamba kwa miaka ya karibuni amekuwa miongoni mwa wanamichezo nguli walioandika kitabu cha maisha yao na kubainisha kwamba kitabu hicho kitawekwa kwenye makataba ya ANOCA, huko Abuja Nigeria yalipo makao makuu kama kumbukumbu.

"Hii ni hatua nzuri kwa mchezaji, pia ni kumbukumbu kubwa," amesema Berraf wakati akipokea kitabu hicho akiwa sanjari na mhazini mkuu wa Heshima ANOCA, Habu Gumel na katibu Mkuu, Ahmed Hashim.

Akizungumzia mkutano huo, Bayi ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania amesema ulilenga kutambua mipango mikakati ya Kamati za Olimpiki Afrika, lakini pia kupata fursa ya kumkabidhi rais wa ANOCA kitabu hicho.

Amesema katika mkutano huo ulioshirikisha makatibu wakuu wa kamati za Olimpiki, ulilenga kuweka mikakati ya Olimpiki kwa nchi za Afrika.

"Kikubwa ilikuwa ni kuangalia ni namna gani tunakwenda kwenye utekelezaji wa mipango hiyo, kwani nchi inaweza kuwa na mipango mizuri lakini ikakwama kwenye utekelezaji.

"Hivyo kila nchi ilichangia kuhusu mipango mikakati ya muda mrefu na mfupi, pia changamoto za utekelezaji wa mipango hiyo," amesema Bayi

Chanzo: Mwanaspoti