Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Polisi warudi na ushindi mashindano Rwanda

RT ERR MAMBOSASA.jpeg Polisi warudi na ushindi mashindano rwanda

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Judo ya Jeshi la Polisi imefanikiwa kutwaa ubingwa wa jumla wa mchezo wa Judo kwa mashindano ya shirikisho la wakuu wa Polisi ukanda wa Afrika Mashariki iliyofanyika Nchini Rwanda Kuanzia march 21 hadi 27 mwaka huu.

Akiongea leo Aprili 13, 2023 mara baada ya ukabidhi kikombe hicho kwa Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt Lazaro Mambosasa Kocha huyo konstebo wa Polisi Zaidi khamisi amesema walijianda vyema na kudumisha nidhamu katika mchezo huo kitendo kilichopelekea kutwaa ushindi na kupata kikombe cha ushindi katika mashindano ya shirikisho la wakuu wa Polisi Nchini Rwanda.

Aidha kocha huyo amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP CAMILIUS WAMBURA kwa namna alivyowawekea mazingira mazuri katika maandalizi yao kuelekea mashindano hayo Nchini Rwanda ambapo umepelekea kuutwaa ubingwa huo.

Sambamba na hilo kocha huyo amemshukuru pia mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Dkt Lazaro Mambosasa kwa kuwapa eneo la kufanya maandalizi ya mashindano yao katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kabla ya Kwenda kushiriki mashindano ya shirikisho la wakuu wa Polisi ukanda wa afrika mashariki yani Police EAPCCO GAMES ambayo yamefanyika nchini Rwanda na kuhusisha nchi saba.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dkt. LAZARO MAMBOSASA amewapongeza na kuwashukuru askari hao walioshiriki vyema mashindano na kutwaa ubingwa huo.

Daktari Mambosasa amesema mbali na kutwaa ubingwa huo amebainisha kuwa ubingwa huo unaitangaza nchi na Jeshi la Polisi kimataifa ambapo amewaomba kuendelea kushiriki kikamilifu kwa mashindano makubwa yajayo na kutwaa ubingwa ili kuipa Nchini sifa katika Medani za kimichezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live