Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Mwendesha baiskeli maarufu duniani Chris Froome kushiriki mashindano Rwanda

Mwendesha Baiskeli Maarufu Duniani Chris Froome Kushiriki Mashindano Rwanda Mwendesha baiskeli maarufu duniani Chris Froome kushiriki mashindano Rwanda

Thu, 16 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Mwingereza mzaliwa wa Kenya amewasili mjini Kigali leo Alhamisi kushiriki mashindano ya baisikeli ya Tour du Rwanda kwa mara yake ya kwanza, alisema alipowasili katika uwanja wa ndege.

Chris Froome, 37, anagombea timu ya wataalamu ya Israeli Premier Tech ambayo pia inatekeleza mradi wake wa mbio za "kubadilisha ulimwengu unaotuzunguka kuwa bora".

"Nimesikia [Rwanda] ni mojawapo ya nchi zinazoongoza katika nchi za Afrika kwa masuala ya uendeshaji baiskeli, ninafurahia kuwa hapa wiki hii kujionea," Bw Froome aliwaambia waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Kigali alipowasili.

Toleo la 15 la Tour du Rwanda, mbio za kilomita 1,130 katika hatua nane zinazoanza Jumapili, zimevutia timu 14 za mashujaa na bara, na timu sita za kitaifa: Algeria, Eritrea, Morocco, Afrika Kusini, Uingereza, na wenyeji Rwanda.

Bw Froome anachukuliwa kuwa mmoja wa waendesha baiskeli mashuhuri, baada ya kushinda mataji ya mbio za baiskeli ikiwa ni pamoja na Grand Tours; nne Tour de France, moja Giro d'Italia, mara mbili ya Vuelta ya Uhispania na mashindano mengine mengi ya kimataifa,

Chanzo: Bbc