Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Mtanzania aibuka kidedea michezo ya madola

Muogeleaji Pic Muogeleaji wa Tanzania, Collins Saliboko

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muogeleaji wa Tanzania, Collins Saliboko amemaliza wa kwanza kwenye kundi lake katika mchujo wa kutafuta tiketi ya kuingia hatua ya 16 bora kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola inayoendelea nchini Uingereza.

Collins amekuwa mchezaji wa kwanza Watanzania kuchuana katika michezo hiyo, huku baadae usiku wa leo bondia Alex Isendi akitarajiwa kupanda ulingoni.

Mpiga mbizi huyo ameanza kwa kuchuana kwenye mtindo wa butterfly mita 50 na kumaliza kwa sekunde 25:52, akiwa nyuma kwa sekunde 3:25 kufikia muda wa dunia ambao ni sekunde 22:27 wakati rekodi ya Jumuiya ya Madola ni sekunde 22:93.

Akiwa kwenye kundi namba tatu, Collins aliwaacha washindani wengine saba kutoka mataifa mbalimbali na kuongoza katika kundi lake.

Hata hivyo muogeleaji huyo atasubiri matokeo ya makundi mengine sita ili kuona kama muda wake umemruhusu kutinga hatua ya 16 bora au vinginevyo kulingana na kanuni na taratibu za mchezo huo.

Waogeleaji 16 wenye muda mkali watashindanishwa katika makundi mawili na wanane watakaokuwa na muda mkali ndiyo wataingia kwenye fainali ili kusaka bingwa katika mtindo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live