Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Mo Farah, Nyota wa riadha aliebadili jina kuingia Uingereza

Sir Mo Jina halisi la Sir Mo Farah ni Hussein Abdi Kahin

Wed, 13 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha wa Uingereza na mshindi wa Medali 4 za Olimpiki Sir Mo Farah amefichua kuwa aliingia nchini Uingereza kwa njia haramu kinyume na sheria na Jina la Mohamed Farah si jina lake halali alipewa jina hilo wakati anaingia Uingereza na jina lake halisi ni Hussein Abdi Kahin.

"Watu wengi wananijua kama Mo Farah, lakini sio jina langu. Hadithi halisi ni kwamba nilizaliwa kaskazini mwa Somalia, kama Hussein Abdi Kahin. Licha ya kile nilichosema katika siku za nyuma, wazazi wangu hawakuwahi kuishi Uingereza. Nilipokuwa na umri wa miaka 4, Baba yangu aliuwawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe (Somalia). Nilitenganishwa na Mama yangu, na nililetwa Uingereza kinyume cha sheria chini ya jina la mtoto mwingine aitwaye Mohamed Farah." Amesema Mo Farah

Sir Mo Salah ni mwengereza wa kwanza kushinda Medali 4 za dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki amesema historia yake ya utotoni ndio iliyomsukuma kupata mafanikio hayo. Sir Mo pia ameshinda medali 6 za dhahabu kwenye michuano ya Dunia ya riadha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live