Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Michezo ya Jumuiya ya Madola haina uhakika kufanyika

Michezo Ya Jumuiya Ya Madola Haina Uhakika Kufanyika Michezo ya Jumuiya ya Madola haina uhakika kufanyika

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2026 haina uhakika wa kufanyika baada ya jimbo la Victoria la Australia kufutilia mbali mipango yake ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kutokana na kuporomoka kwa bajeti.

Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola (CGF) lilitatizika kupata mwenyeji kabla ya jimbo la Victoria kujitolea mnamo Aprili 2022.

Lakini Waziri Mkuu alisema gharama iliyokadiriwa sasa imeongezeka mara tatu na kuwa "ghali mno" kwa serikali kubeba mzigo huo.

Shirikisho hilo liliita uamuzi huo "wa kukatisha tamaa sana" na kusema "imejitolea kutafuta suluhu".

Michezo ya Jumuiya ya Madola imewahi kufutwa tu wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.

Mkuu wa jimbo la Victoria Daniel Andrews Jumanne alisema Victoria alikuwa "mwenye furaha kusaidia" alipofikiwa kuwa mwenyeji mwaka jana, lakini "sio kwa gharama yoyote".

Waandalizi awali walikuwa wamekadiria tukio hilo - lililoandaliwa katika miji yote ikiwa ni pamoja na Geelong, Bendigo na Ballarat - lingegharimu A $2.6 bilioni (£1.4bn; $1.8bn) na serikali ya jimbo ilikuwa imechukulia kama faida kwa mikoa.

Chanzo: Bbc