Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Mashindano ya riadha ya kubeba wake zao

Mashindano Ya Riadha Ya Kubeba Wake Zao Mashindano ya riadha ya kubeba wake zao

Tue, 6 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chukua hii, nchini Finland kuna mashindano ya wanaume kubeba wake zao mgongoni au shingoni kisha kukimbia nao na mshindi kupewa fedha taslimu pamoja na bia zenye idadi sawa na uzito wa mke husika.

Huko Finland mashindano hayo yalianza mnamo karne ya 19 na kuwa mchezo rasmi mwaka 1992 huku baadaye wakiruhusu raia wa nchi zingine kushiriki mwaka 1995.

Mchezo huo ambao umetokea kupendwa na wengi hadi kupewa hadhi ya kimataifa, unahusisha wapenzi au wanandoa na lazima mke atakaye bebwa awe wa mwanaume husika.

Pamoja na hayo, mwanamke atakayebebwa atatakiwa kuwa na uzito usiopungua kilo 49 na kama itakuwa pungufu basi itabidi afungashiwe mzigo ili uzito wake ufikie kilo 49.

Mshindi hupatikana kwa mwanaume aliyeweza kukimbia kwa kasi zaidi na mkewe kichwani na zawadi kuu ambayo ni pombe itatolea kwa katoni sawa na uzito wa mke wake kwa kutumia mzani maalum yaani 'bembea'.

Je, Tanzania itatoboa na mashindano haya?????????

Chanzo: www.tanzaniaweb.live