Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Kocha wa Simbu kuzikwa leo Arusha

Simbu Ds Kocha wa Simbu kuzikwa leo Arusha

Wed, 26 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa Francis John, aliyekuwa kocha wa mwanariadha, Alphonce Simbu, utazikwa leo Aprili 26 nyumbani kwake jijini Arusha.

Francis alifariki jioni ya Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari.

Simbu ameiambia Mwananchi Digital kuwa maziko ya kocha huyo yatafanyika kwenye eneo la nyumba yake huko Arusha, mchana huu.

Hadi mauti inamkuta, Francis alikuwa kocha binafsi wa mwanariadha huyo ambaye pia ni mshindi wa medali ya shaba ya Jumuiya ya Madola.

Mbali na ukocha, Francis amewahi kuwa mwenyekiti wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live