Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Jeshi Stars, Uhamiaji hatarini kushushwa daraja

Cb31aaf3c259b151937ef27ae2f4e7c9.jpeg Jeshi Stars, Uhamiaji hatarini kushushwa daraja

Mon, 11 Jul 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wakongwe wa netiboli nchini, Jeshi Stars na Uhamiaji ni miongoni mwa timu zilizoko katika hatari ya kushushwa daraja baada ya kushindwa kushiriki Mashindano ya Klabu Bingwa ya netiboli yaliyoanza juzi kwenye Uwanja wa Taifa wa Ndani.

Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Rose Mkisi akizungumza na habari leo katika mahojiano maalum jana alisema kuwa Jeshi Stars na Uhamiaji pamoja na kuthibitisha kushiriki, bado hazijalipa ada. Alisema kuwa katika uongozi wake timu zote ni sawa na hatakubali kuona timu zinathibitisha kushiriki, lakini zinashindwa kulipia ada na kutotokea katika mashindano hayo.

Mkisi aliyeingia madarakani katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni alizitaka timu zingine, ambazo huenda zikakumbwa na panga hilo ni Polisi Tanga, Polisi Kigoma, Mbeya City, JKT Mgulani, JKT Makutupola, Ihumwa na MVRF ya Mabibo. Alisema kuwa timu hizo zimepewa hadi kesho ziwe zimelipa ada nakushiriki mashindano hayo yaliyoanza juzi kwenye uwanja huo.

Alisema kila timu inatakiwa kulipa kiasi cha Sh 500,000 ada ya ushiriki wa mashindano hayo, ambayo hutoa bingwa wa Tanzania Bara, ambaye pamoja na washindi wengine wawili, hushiriki Mashindano ya Muungano ambayo hushirikisha na timu za Zanzibar.

Timu ambazo zinachuana katika mashindano hayo ni mabingwa watetezi JKT Mbweni, Tamisemi Dodoma, Magereza na Polisi zote za Morogoro, Polisi Arusha, Eagle Queens, Kampala University na UDSM.

Chanzo: www.habarileo.co.tz