Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Bingwa wa dunia wa Marathon Kelvin Kiptum afariki

Bingwa Wa Dunia Wa Marathon Kelvin Kiptum Afariki Bingwa wa dunia wa Marathon Kelvin Kiptum afariki

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: Voa

Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia ya mbio za marathon Kelvin Kiptum na kocha wake Gervais Hakizimana walifariki katika ajali ya barabarani siku ya Jumapili, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Waziri wa michezo wa Kenya, Ababu Namwamba alisema kwenye X , "Inauma sana!! Kenya imepoteza mtu mwenye thamani maalum. Sijui nisema nini."

Kiptum, aliyekuwa na umri wa miaka 24, aliweka rekodi ya dunia katika mbio za Chicago Marathon, mwezi Oktoba mwaka jana, kwa muda wa saa mbili na nukta 35 na kuvunja rekodi ya iliyokuwa imewekwa na mwenzake Eliud Kipchoge mjini Berlin mnamo mwaka 2022.

Kiptum alivunja rekodi ya London Marathon mapema mwaka jana na alidhamiria kufanya vivyo hivyo tena mjini Chicago, ambako alikimbaia umbali wa kilomita 35 kabla ya kuinua mikono yake hewani huku akishangiliwa na umati wa watu chini hadi pale aliposhinda mbio hizo.

Chanzo: Voa