Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Betras kinara kikapu U-23

Kikapu1 Betras kinara kikapu U-23

Wed, 7 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya mpira wa kikapu ya Betras inaendeleza ushindi katika mashindano ya vijana walio chini ya umri wa miaka 23 baada ya kuifunga Sixers kwa pointi 79-66 katika Uwanja wa Maisara, Zanzibar.

Katika mchezo huo kila upande ulionekana kuwa na ushindani mkali uliotoa burudani tosha machoni mwa mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo.

Betras ambao ni ushindi wake wa tatu mfululizo toka kuanza kwa mashindano hayo yenye lengo la kukuza vipaji vya vijana, ilionesha dalili za mapema kushinda kutokana na kuutawala kila idara.

Michuano hiyo leo inatarajiwa kuendelea tena kwa kuchezwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Polisi na Usolo timu ambazo zote zimepoteza michezo yao miwili ya awali.

Wakati huo huo Ligi Kuu ya soka la wanawake Zanzibar inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 7 kwa kuchezwa mchezo mmoja utakaowakutanisha Warriors na timu ya Umoja wa Makundi Zanzibar (UMZ).

Mchezo huo wa ufunguzi unatarajiwa kushuhudiwa na Katibu wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), Said Marine ambaye ndiye mgeni rasmi.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo inayoshirikisha timu saba, michezo yote itakuwa ikichezwa katika Uwanja wa Mao Zedong.

Aidha, ratiba hiyo inaonesha Desemba 8 uwanjani hapo kutapigwa mchezo mmoja pia kati ya P.D.S na Green Queen, wakati Ijumaa Dunga Queen itapambana na New Gere. Timu nyingine zinazoshiriki ligi hiyo ni New Generation na Yellow Queen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live