Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Bendera ya Urusi haina nafasi Michezo ya Olimpiki ya Paris-Macron

Bendera Ya Urusi Haina Nafasi Kwenye Michezo Ya Olimpiki Ya Paris Macron Bendera ya Urusi haina nafasi Michezo ya Olimpiki ya Paris-Macron

Thu, 7 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Bendera ya Urusi haina nafasi katika Michezo ya Olimpiki mjini Paris wakati Urusi ikifanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema katika mahojiano gazeti la michezo la Ufaransa L'Équipe.

"Ni wazi, hakuwezi kuwa na bendera ya Urusi kwenye Michezo ya Paris, nadhani kuna makubaliano juu ya hili," Macron alisema. "Urusi kama nchi haina nafasi wakati inatenda uhalifu wa kivita na kuwafukuza watoto."

Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa ilipendekeza kuruhusu wanariadha kutoka Urusi na Belarus kushindana katika mashindano ya kimataifa katika hali ya kutokuwa na upendeleo katika taaluma za mtu binafsi.

Wanariadha pia wanahitaji kutimiza masharti fulani: hususan hawakupaswa kuunga mkono uvamizi wa Urusi kwa Ukraine na kuwa na uhusiano na jeshi la Urusi au Belarusi, na vile vile vikosi vya usalama vya nchi zote mbili.

"Suala ambalo ulimwengu wa Olimpiki unapaswa kuamua ni mahali gani pa kuwapa wanariadha wa Urusi, ambao wakati mwingine wamekuwa wakifanya mazoezi maisha yao yote [kwa ajili ya mashindano] lakini wanaweza kujikuta wahanga wa utawala huu," Macron aliiambia L'Équipe.

Kwa mujibu wa Macron, ni muhimu kutofautisha kati ya wanariadha ambao kwa kweli wanahusika katika vitendo vya mamlaka ya Urusi na wale ambao ni waathirika wa utawala. Kwa maana hii, IOC lazima ifanye uamuzi ambao wa haki na unaoeleweka kwa Waukraine.

"Huu ndio usawa ambao tunapaswa kuhakikisha," rais wa Ufaransa aliongeza.

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto itafanyika mjini Paris kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, 2024.

Chanzo: Bbc