Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Bangi yamponza mshindi wa medali ya dhahabu Olympic

Joseph Schooling.jpeg Bangi yamponza mshindi wa medali ya dhahabu Olympic

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshindi wa kwanza wa Medali ya dhahabu ya Olimpiki nchini Singapore, Joseph Schooling (27) amesimamishwa kushiriki mashindano yeyote ya kuogelea, baada ya kukiri kutumia bangi akiwa Vietnam mwezi Mei.

"Nilionyesha tabia mbaya na ninaomba radhi, nimeiumiza familia yangu na mashabiki vijana waliokuwa wakinitazama mimi kama mfano,” amesema Schooling.

Muogeleaji huyo alikuwa shujaa wa michezo alipoishindia nchi yake medali ya kwanza ya dhahabu katika mashindano ya Rio mwaka 2016.

Kashfa hii imegawanya maoni ya watu katika nchi hiyo ambayo inajulikana kwa sheria kali juu ya dawa za kulevya ambapo hukumu yake hufikia hadi miaka 10 jela na faini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live