Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Australia: Aweka rekodi ya kupiga ‘push ups’ 3,200 kwa saa moja

Pushuppp Australia: Aweka rekodi ya kupiga ‘push ups’ 3,200 kwa saa moja

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lucas Helmke (33) amevunja rekodi iliyowekwa na raia mwenzake wa #Australia, #DanielScali aliyepiga ‘push ups’ 3,182, Aprili 2022

Kufikia viwango na kuingizwa kwenye rekodi za #Guinness, kila ‘push up’ ilibidi isiwe na dosari akitakiwa kuuweka sawa mwili kuelekea juu, kutokunja magoti na kiuno, akitakiwa kufikia angalau pembe ya digrii 90 kwenye kiwiko cha mkono anaposhuka.

Lucas Helmke (33) ameweka rekodi hiyo katika ukumbi wake wa mazoezi uliopo Brisbane kuvunja rekodi iliyowekwa na raia mwenzake wa Australia, Mwaka 2022.

Kila push up ilibidi isiwe na dosari ili kufikia viwango vinavyohitajika kwa rekodi rasmi ya Dunia, akitakiwa kuuweka sawa mwili wake akielekea juu, bila kukunja magoti na kiuno, huku akifikia angalau pembe ya digrii 90 kwenye kiwiko cha mkono anaposhuka.

Rekodi hiyo iliyoingia kwenye Kumbukumbu za Guinness awali ilikuwa ikishikiliwa na Daniel Scali aliyepiga push ups 3,182, Aprili 2022.

Helmke amesema imemchukua miaka mitatu kitengeneza mwili kuwa fiti kuweza kuvunja rekodi hiyo.

Kabla ya kufanya zoezi hilo Helmke alitoa taarifa kwa Guinness World Records kuwa anataka kuweka rekodi hiyo kwa ajili ya mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live