Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Apotea akisafiri kwa miguu

Santiago Sanchez .jpeg Apotea akisafiri kwa miguu

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhispania aliyeamua kutembea kwa miguu kutoka jijini Madrid kuelekea Doha kwa ajili ya Kombe la Dunia 2022, amepotea.

Mnamo mwezi Januari, Santiago Sanchez aliianza safari hiyo ya kilomita 6,800 ambayo ingemchukua miezi 11.

Kwa mujibu wa gazeti la El Mundo, mnamo Oktoba 2, baada ya kupita nchi kadhaa za Ulaya na Asia mawasiliano na Sanchez yalikatika. Wakati huo alikuwa akiukaribia mpaka wa Iran.

Familia yake ilishikwa na wasiwasi kwa kimya chake na kuamua kuanza kumtafuta. Mara ya mwisho alizungumza na rafiki yake Oktoba 1 na alituma ujumbe kwa njia ya WhatsApp Oktoba 2.

Kutokana na machafuko ya kisiasa yanayoendelea Iran, huenda ameshikiliwa na polisi, hata hivyo jambo hilo halina uhakika na mamlaka husika zinaendelea kumtafuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live