Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Various Sports

Aliyeshindwa awa shujaa Olympic 2024

Kinzang Lhamo 1200x675 Kinzang Lhamo

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha Kinzang Lhamo wa nchi ya Bhutan amemaliza nafasi ya 80 katika marathon ya Olimpic jana, akitumia saa 3:52:59 wakati mshindi wa kwanza Sifaa Hassani wa Uholanzi akitumia saa 2:22:59 na wa 79 Sherstha wa Nepal akitumia 2:55:06.

Pamoja na kumaliza nafasi hiyo, amekuwa kivutio kikubwa kwenye mbio hizo, kwani hakukata tamaa licha ya saa 1 kupita tangu wenzake wamalize mbio yeye aliendelea kukimbia peke yake.

Haya ni matokeo mabaya kwa Lhamo kwa sababu muda wake bora katika km 42 ni saa 3 na dakika 26 lakini jana amebeba ushujaa kama mwanariadha wa Tanzania John Akhwari kwenye olimpic mwaka 1968, ambaye alipata majeraha na kuvuja damu kwenye goti lakini aliendelea kukimbia pamoja na wenzake mpaka anamaliza walikuwa tayari washamaliza zoezi la kuwapa medali.

Mwanariadha Kinzang Lhamo ameshiriki Olimpic mwaka huu kwa tiketi ya universality(hakufuzu) kuiwakilisha nchi ya nchi yake ya Bhuyan yenye wakazi laki 7 iliyopo mashariki mwa safu za milima ya Himalaya.Kwa upande wa Kaskazin kuna nchi ya China na Kusini India.

Mwanariadha huyu pia ni mwanajeshi wa nchi ya Buthan amekuwa shujaa aliyeshindwa na kuitangaza nchi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live