Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Martial Arts

Tashoka yatekeleza kwa vitendo

IMG 1207 640x423 Wachezaji wa Karate

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Chama cha Mchezo wa Karate Tanzania (TASHOKA) kinaendelea kutekeleza kwa vitendo matukio katika kalenda yake ya Mwaka 2022 iliyoitoa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Kalenda hiyo Kuanzia Februari 12 mpaka April 16 mwaka huu kunafanyika semina elekezi kwa wakufunzi wote wa vilabu Vya Tashoka pia kunafanyika kozi ya urefa wa Karate Grade D,C na B.

Katibu mkuu wa Chama cha Mchezo wa Karate Tanzania Sensei Jerome Mhagama,amesema sehemu zitakazohusika na semina na kozi hizo ni Dar es Salaam,Singida na Iringa.

Kalenda hio ni rasmi ya Tanzania Shotokan-Ryu Karate-DO Association (TASHOKA) itakayo tumika kwa kipindi chote cha Mwaka-2022.

Kwa kuzingatia kuwa Kalenda nyingi za Mashirikisho ya Kimataifa bado hazijawa tayari mpaka hivi sasa na kwa kawaida Kalenda nyingi za Mashirikisho hayo zinatoka mwezi Machi-2022, hivyo basi yapo katukio mengi ya Kimataifa ambayo hayapo katika Kalenda kwa sasa.

Kwa msingi huo kama Taifa tunaweza kupata mualiko wa tukio lolote la Kimataifa ambalo halipo katika Kalenda kwa sasa na kupelekea mabadiliko ya Kalenda yetu kwa wakati wowote kuanzia mwezi Machi, na hii itakuwa kwa yale matukio yenye tija kwa Taifa tu.

Chanzo: eatv.tv