Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Martial Arts

Tanzania yakosa medali ya kwanza Olympic

Andrew Mlugu.jpeg Tanzania yakosa medali ya kwanza Olympic

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kuanza vyema kwa kuibuka na ushindi katika hatua ya 32 kwenye mchezo wa Judo, Mtanzania Andrew Mlugu amepoteza pambano lake la hatua ya 16 bora dhidi ya Joan-Benjamin Gaba na kuikosesha Tanzania medali ya kwanza kwenye michezo hiyo.

Baada ya kupita raundi ya 64 bora bila kucheza, matumaini ya Tanzania kupata medali kupitia kwa Mlugu yalikuwa makubwa baada ya mcheza judo huyo kuibuka na ushindi wa pointi 10-1 dhidi ya William Tai Tin wa Samoa.

Hata hivyo alijikuta akipoteza pambano la raundi ya 16 bora dhidi ya Gaba wa Ufaransa kwa kuchapwa pointi 10-0 na hivyo kuaga mashindano hayo.

Baada ya Mlugu kuambulia patupu, matumaini ya Watanzania sasa yamehamia kwa wakimbiaji Gabriel Geay, Alphonce Simbu, Jackline Sakilu na Magdalena Shauri pamoja na waogeleaji Collins Saliboko na Sophia Latiff.

Kesho, Saliboko ataiwakilisha Tanzania wakati atakapokata maji kwenye mita 100 free style na Ijumaa ijayo, Latiff atapeperusha bendera katika mita 50 free style.

Hadi sasa, Marekani ndio inaongoza kwa kutwaa medali ikiwa nazo 12 ikifuatiwa na China iliyokusanya tisa.

Ufaransa ina medali nane na Japan na Korea Kusini kila moja ina medali saba kibindoni.

Nchi ambazo zina medali sita kila moja ni Australia na Italia wakati Uingereza ikiwa na medali tano.

Canada, Brazil na Kazakhstan kila moja ina medali tatu na Ubelgiji ina medali mbili huku nchi zenye medali mojamoja zikiwa ni Ujerumani, Hong Kong na Uzbekistan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live