Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Martial Arts

Shotokan Karate wameibuka na ushindi wa tatu

WhatsApp Image 2022 05 30 At 5.14.05 PM.jpeg Mchezaji wa Shotokan Karate

Tue, 31 May 2022 Chanzo: eatv.tv

Wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo wa Shotokan Karate wameibuka na ushindi wa tatu (3) katika mashindano ya Kanda ya tano (Zone 5) yanayoandaliwa na Shirikisho la Afrika la mchezo huo waliyoshiriki kama waalikwa, mashindano yaliyofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 22 Mei, 2022 nchini Kenya.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Chama cha mchezo huo nchini (TASHOKA) Jerome Mhagama kwa njia ya simu wakati timu ikiwa njiani kurejea nchini.

"Awali ya yote tunamshukuru sana Mungu kwa kutusimamia katika safari yetu na kumaliza salama Mashindano kwa ushindi wa nafasi ya tatu kwa Team KATA (3 Bronze Medals), nafasi ya kwanza imechukuliwa na Madagasca na nafasi ya pili ni Kenya,"alisema Mhagama na kuongeza kuwa;

"Vijana walipambana kwa moyo sana na kwa uzalendo mkubwa hadi kushika nafasi hii baada ya kuzishinda nchi za Ethiopia, Uganda, Burundi, Somalia, Sudan, South Sudan, Seychelles, Comoros, Mauritius, Djibouti, Eritrea na Rwanda,"alieleza

Aidha, Mhagama alieleza kuwa timu yao ilishiriki kama waalikwa kwa heshima ya umaarufu na mchango wa nchi ya Tanzania kwa Nchi nyingi za Afrika na huku akisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha mashirikisho ya michezo na siyo vyama kama walivyoshiriki wao.

"Tumeitumia fursa hii kujifunza mambo mengi, pamoja na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wa ngazi za juu wa UFAK (Union Of Africa Karate Federations) na kuweka mazingira ya tutakapo pata federation yetu wawe tayari kuipokea Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASHOKA na mwalimu wa mchezo huo Yahaya Mgeni ameshukuru ushirikiano wa Serikali kupitia Wizara, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Ubalozi wa Tanzania Nchini Kenya na Watanzania kwa dua na ufuataliaji wa karibu wa mashindano hayo.

"Mama ameupiga sasa, maana ya kuupiga sana sisi tumekuja Kenya kwa ufadhili wa Serikali kupitia BMT, tunamwahidi Mama hatutamwangusha,"alisema Mgeni.

Timu iliwakilishwa na wachezaji 6 wa Michezo ya Mtu mmoja mmoja (Individual Game) aina ya kumite wanne na Kata wawili.

Chanzo: eatv.tv