Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Martial Arts

Mke amfungulia mashtaka mumewe kwa madai yanayohusu watoto wao

2868 Man Arrested

Fri, 9 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Kutoka Kenya tukiachana stori zinazomhusu aliyemuapisha Raila Odinga, Miguna Miguna kuna hii inayomhusu Mwanaume mmoja raia wa Kenya aliyetambulika kwa jina la Samwel Kago mwenye miaka 48 Jumatano January 7, 2018 alikamatwa na polisi kwa kosa la kutowapeleka watoto wake wawili shule.

Winnie Kago ambaye ni mke wa Mwanaume huyo ndiye aliyekwenda polisi na kumshtaki mumewe kwa kutopeleka watoto wao shule ingawa amedai kuwa anauwezo wa kutosha wa kufanya hivyo.

Kwenye mashtaka hayo ameeleza kuwa mwanaume huyo amekuwa akimlazimisha kutumia pesa zote anazozipata kwenye biashara zake ndogondogo kulisha familia na kulipia gharama za mahitaji yote ya familia ikiwa naye ana kipato.

Winnie ameongeza pia kuwa mtoto wao wa kwanza ana miaka 15 alifanya mtihani wa kumaliza elimu yake ya msingi tangu mwaka 2016 lakini hadi leo bado hajaanza kusoma Sekondari wakati mtoto wao wa pili alianza masomo ya awali mwaka jana lakini imebidi aachishwe shule kutokana na baba huyo kukataa kulipa ada.

BREAKING: DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOFIKA MAHAKAMANI KISUTU LEO

LIVE BUNGENI: Kipindi cha maswali na majibu



Wema Sepetu alivyofika Mahakamani Kisutu na Wakili Msando

Chanzo: millardayo.com