Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Martial Arts

Michezo ya mapigano yapamba moto

Mapigano Sanaa Michezo ya mapigano yapamba moto

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: eatv

Wachezaji 40 wa sanaa za mapigano wanatarajia kushiriki Ligi ya Fay herous ambayo itaanza Februari 25 mwaka huu kwenye fukwe ya Azura Dar Es Salaam.

Ligi hiyo imeandaliwa na Chama cha Wushu(TWA) Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Kusimamia ngumi za Kulipwa Tanzania ( TPBRC) na Klabu ya Fay Herous.

Katibu Mkuu wa TWA Sensei Gola Kapipi ,alisema kuwa wachezaji hao ni WA michezo ya ngumi za Kulipwa ,kickboxing Judo ,Karate na Wushu.

"Ligi Hii itakuwa inafanyika kila mwezi na tunatoa Fursa kwa michezo ambayo haifanyi mashindano iweze kutoa nafasi ya Vijana kushiriki waweze kujitengenezea kupata ajira na kuinua michezo hiyo," alisema Sensei Kapipi.

Naye Katibu Mkuu wa TPBRC Yahya Poli,alisema kuwa kwa ngumi za Kulipwa itashirikisha mapambano tisa kati ya hayo yapo ya Wanawake.

'' lengo ni kukuza,kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia mchezo huo''Katibu Mkuu wa TPBRC Yahya Poli

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Uhusiano na mawasiliano wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT ) Najaha Bakari,aliwaomba wadau na wadhamini kujitokeza kuunga mkono kwa kusaidia kufanikisha Ligi hiyo.

Wito mwingine kwa waandaji kuendelea kuandaa mashindano mengi Ili kutoa fursa kwa wachezaji kushiriki na kuibua vipaji mtaani Ili kuweza kupata wawakilishi bora kimataifa.

Chanzo: eatv