Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Martial Arts

Karate Tanzania kushiriki Maziwa makuu

IMG 6117 1140x640 Karate Tanzania kushiriki Maziwa makuu

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: Dar24

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mchezo wa Karate itashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Nchi za maziwa Makuu nchini Kongo yanayotarajiwa kuanza kutimua Vumbi Kuanzia Tarehe 17 mpaka 23 mwezi huu.

Timu ya Tanzania yenye wachezaji 20 kutoka mikoa mbalimbali nchini humo,itashiriki katika Mashindano hayo yatakayohisisha nchi zaidi ya 14, Kongo , Angola,nchi za ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na nchi Alikwa.

Hii ni Mara pili kwa Tanzania kushiriki mashindano hayo,Mara ya kwanza ni mwaka 2021, ambapo Tanzania Ilikamata nafasi ya pili kwa Ushindi wa Jumla, huku Kongo wakiwa wa kwanza.

Tanzania ilipata nafasi hiyo baada ya kuzishinda nchi za Ethiopia, Uganda, Burundi, Somalia, Sudan, South Sudan, Seychelles, Comoros, Mauritius, Djibouti, Eritrea na Rwanda.

MAJINA

1.Yahya Mgeni-Rais wa Shirikisho la Karate Tanzania

2. Lawrence Mapunda -Katibu Kamati ya Ufundi Shirikisho la Karate Tanzania

3.Scola Peter -Mchezaji Timu ya Karate Tanzania

4.Petro Lucas Madai –Nahodha Timu ya Tanzania (Kumite)

Chanzo: Dar24